IBADA YA JUMAPILI TAR 07/08/2016
KANILA LA ANGLIKANA TANZANIA
DAYOSISI YA RUVUMA
KANISA LA MT. AGUSTINO-MTAA MJIMWEMA SONGEA
SOMO: REHEMA ZA MUNGU
MHUBIRI Mwl. PETER MAKWENDA
SEHEMU YA I
Utangulizi
Chukua
mfano wa mwanafunzi aliyefanya kosa shuleni, halafu kama mwalimua au
mzazi ukamchukua ukamhoji, je kwa nini umefanya hivi, atakuambia mwalimu
(au mzee) mimi sijafanya hili na unajua kabisa aliyefanya jambo hili ni
Simon( mfano), unamuambia Simon hebu niambie kwa hakika ni nani
amefanya hili kama si wewe, atakuambia Baba unajua tulikuwa tunacheza
tu, kwa bahati mbaya tukadondosha TV ikapasuka, au mwalimu sikuwa
nimedhamiria kuumiza ila tulikuwa tunacheza nikamrushia kalamu ndio kwa
bahati ikamchoma kwenye jicho, baada ya huyu mtu kufahamu kosa
alilolifanya ataomba msamaha na akishapewa msamaha atapewa kazi ya
kufanya, mwingine anaweza pewa eneo la kufyeka au kwa sababu umemuumiza
mweza hautopewa pocket money kwa muda wa week 3 au kutohudhuria michezo
kwa muda wa mwezi mmoja
Na baba
yetu pamoja na mama yetu, Adama na mkewe Hawa walipofanya kosa walipewa
msamaha lakini kuna jambo la kufanya walipewa wakaambiwa (Mwa 3:17)
“... kwa jasho la uso wako utakula Chakula ....” Sasa ile adhabu
inaposimama ndipo tunapoanza kutazama upande wa pili wa rehema.
Sasa
je, Rehema ni kitu gani? Tunasema kwa lugha rahisi kwamba rehema ni
ondoleo la adhabu baada ya kosa au inayoambata na kosa kupewa msamaha.
Kosa linapofanyika linatanguliwa na msamaha halafu rehema ndipo
inaposimama, kwa hiyo rehema inasimama kutuondolea adhabu baada ya sisi
kusamehewa makosa yetu
. Ukisoma kitabu cha Kut 20:4-6 “ ... ni Mungu
nwenye wivu, nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu
na cha nne cha wanichukiao, name nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na
kuzishika amri zangu”. Maandiko yanasema kosa linapofanyika halafu mtu
asipotubu lile kosa, au msamaha unapotoka halafu lile lililotolewa
msamaha halijafanyiwa, kazi basi kosa hilo linapatilizwa kwa wana hata
kizazi cha tatu hata cha nne cha wote wenye kumchukia MUNGU
SEHEMU YA II
Sasa
Je, rehema inakuja wapi? Rehema inakuja ili kusimamisha kule
kupatilizwa kosa kwa ntoto hadi kizazi cha tatu na cha nne, ili kila mtu
abebe mzigo wake MWENYEWE. Ezekiel 17:1-17 “... hatakufa huyu kwa
sababu ya uovu wa baba yake, hakika ataishi” Kwa hiyo rehema inasimama
baada ya mtu ( iwe baba au mama) amejua kosa anaumua kuomba rehema ili
watoto wake wasipatilizwe, akasema nimeamua kumtafuta MUNGU,
akishamtafuta tu REHEMA inaingia kwenye kizazi cha mwana, halafu kizazi
cha tatu, cha nne na kuendelea “maelfu elfu” wampendao MUNGU, badala ya
kupatilizwakosa kinaingia kitu kinachoitwa Baraka, kwa hiyo ili Baraka
iendelee inabidi watu waendelee kumpenda YESU na kuzishika
amri
zake. Kwa tunafahamu sasa kwamba rehema si ya bure, hatuwezi kupata
rehema mpaka bure ila tutapata baada ya kuwa tumefanyaka kazi. Rehema ni
tofauti kidogo na neema, ebu tuangalie kidogo, tunaposema neema
tunamaanisha kustahilishwa kwa mtu asiyestahili, mwanzoni mimi, wewe na
kila mmoja alikuwa ana kosa pamoja na asili ya kufanya dhambi. Kwa hiyo
ile asili ya kufanya dhambi kila wakati ikwa inamvuta mtu aendelee
kufanya dhambi. Anasema katika Yoh 3:16 “ Kwa maana jinsi hii MUNGU
aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila amwaminiye
asipotee bali awe na uzima wa milele”
Kwa
hiyo hatuhitaji kulipa (kitu) ili tupate neema, ila tunahitaji kazi ya
kufanya ili rehema iingie, rehema ili iendelee kukaa tunatakiwa kufanya
kitu. Neema inamuokoa mtu mmoja kwenye familia lakini rehema inaokoa
kizazi ngoja nirudie tena hapa Neema inamuokoa mtu mmoja kwenye familia
lakini rehema inaokoa kizazi hata kizazi, Yohana anaandika maneno ya
YEsu anasema “... ili kila amwaminiye....” Maana yake ni kwamba baba
anaweza kuwa anaamini lakini mama asiamini au baba anaweza kuwa anaamini
lakini mwana asiamini na kwa hiyo baba ataokolewa kwa neema lakini sio
mtoto kwa sababu baba ameokolewa. Lakini Rehema inapoingia Mungu anasema
hivi , “ name nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri
zangu” kwa sabau gani kazi aliyoifanya baba inatembea mpaka kwa mtoto,
leo tunao ujasiri kusema MUNGU wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka na MUNGU wa
Yakobo kwa sababu ya kazi ya mtu mmoja Ibrahimu ambae alikubali
kumtafuta MUNGU na ahadi zake,ndipo rehema za MUNGU kwa Ibrahimu
zikatembea mpaka kwa watoto
Tunasoma
Mazungumzo mazuri sana kati ya MUNGU na Sulemani katika 1 Fal 3;5-15, “
Sulemani akasema, umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu,
kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki ....” Kwa
hiyo MUNGU alimtokea Sulemani si kwa sababu ya Sulemani bali kwa sababu
ya Daudi baba yake
Kwa hiyo
tunaona tofauti kati ya neema inayookoa mtu mmoja na rehema inayookoa
vizazi hata vizazi, ili kizazi kiekae katika Baraka basi unahitaji sana
kukaa katika rehema, ebu tusome kidog Rum8:1 “ sasa basi hakuna hukumu
ya adhabu juu yao walio katika KRISTO YESU” Kwa hiyo rehema inakuja
kusimama badal aya hukumu ya adhabu
Nini tunahitaji ili kusiimamisha Baraka katika vizazi
Rehema
si bure bali inahitaji tufanye kazi ili rehema itembee katika vizazi
vyetu. Mambo yafuatayo ni msingi wa kusimamisha rehema katika vizazi
(i) Yoh 3:16, Yoh 1:12 Kumwamini YESU, huku kunamsogeza mtu na kizazi chake
katika rehema za MUNGU (ii) Yoh 14;15 “ Mkinipenda mtazishika amri zangu” Jambo la pili ni kumpenda
MUNGU
na kushika amri zake (iii) Rum 8:1, “sasa basi hakuna hukumu ya adhabu
juu yao walio katika KRISTO YESU” kukaa ndani ya YESU, kwa YESU ndiko
kwenye rehema kwa hiyo ili kukaa kwenye rehema mtu anahitaji kukaa ndani
ya YESU
Na hizi ndizo faida za MTU kukaa na REHEMA za MUNGU
(a)
Kuondolewa laana za vizazi, Kut 20: 4-6, (b) Kufanikiwa na kuinuliwa
Zab 27;4, 23:6 (c) Kuheshiwa mbele za watu na mbele za MUNGU, Yoh 12: 26
Tamani
sana Kukaa na Rehema za Mungu ili kusimamisha Baraka katika vizazi
vyako na kuona mkono wa MUNGU ukizidi kutembea na wewe, milele yote
MUNGU Mwaminifu, mshika maagano azidi kukubariki
Mwl. Peter Makwenda
+255 754 615213
makwendap@gmail.com
No comments:
Post a Comment