Hippo Parish Mjimwema Songea

Karibu katika tovuti ya kanisa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma, mtaa wa mtakatifu Agustino Hippo Parishi Mjimwema Songea,kwa mawasiliano SLP 600 Songea ,baruapepe ni hippoparish.mjimwema@gmail.com

Friday 29 July 2016

Kanisa la Mtakatifu Agustino wa Hippo Mjimwema

 Kanisa jipya la mtaa wa mtakatifu Agustino wa Hippo Mjimwema Songea,ambalo linaendelea na ujenzi ambapo hadi sasa limegharimu zaidi ya shilingi milioni 50.
Ili kukamilika kanisa hilo zinatarajiwa kutumika zaidi ya shilingi milioni 70.Wote ambao wanaguswa kusaidi ukamilishaji wa kanisa hili,wasiliana na padre wa mtaa kwa simu namba +225764932162,baruapepe hippoparish.mjimwema@gmail.com,akaunti namba benki ya CRDB NO.0152201264100  JINA LA AKAUNTI KANISA LA

Siku ya kumsimika Askofu wa Dayosisi ya Ruvuma


Askofu  mkuu wa kanisa la Anglikana Tanzania Jacob Chimeledya akiwa katika maandamano ya kumsimika Askofu wa nne wa Dayosisi ya Ruvuma Mhashamu Raphael Haule katika kanisa kuu la Msalaba mtakatifu Liuli Nyasa mkoa wa Ruvuma.

Litania ya kumweka wakfu Askofu wa Ruvuma

Hapa ni ndani ya kanisa kuu la Msalaba mtakatifu la Liuli,wakati wa kumweka wakfu Askofu wa nne wa Dayosisi ya Ruvuma mhashamu Raphael Haule aliyelala madhabahuni wakati wa Litania.


Askofu wa Dayosisi ya Ruvuma akisani Hati ya kuwa Askofu

Askofu wa nne wa Dayosisi ya Ruvuma  mhashamu Raphael Haule akisaini Hati ya kukubali kuwa Askofu wa Ruvuma mbele ya msajili wa jimbo profesa John Kabudi Mpalamagamba katika kanisa kuu la Dayosisi ya Ruvuma Liuli.

Vicar General akimsimika Rasmi Askofu wa Ruvuma

Vicar General wa kanisa Anglikana Ruvuma padre Simon Ntauchila akimsimika rasmi Askofu wa nne wa Dayosisi ya Ruvuma katika kanisa kuu la Msalaba Liuli.

Watawa wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma

Hapa ni makao makuu ya kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma wakati wa kusimikwa Askofu mpya wa Dayosisi hiyo mhashamu Raphael Haule Liuli wilayani Nyasa mkoani Ruvuma

Maaskofu waliohudhuria misa ya wakfu

Hapa ni baadhi ya maaskofu kutoka sehemu mbalimbali nchini ambao walihuduhuria misa ya wakfu kwa Askofu wa nne wa kanisa Anglikana Ruvuma